Wahadhiri na wafanyikazi wa chuo kikuu cha Moi waanza tena kugoma

  • | K24 Video
    16 views

    Mwezi mmoja tu baada ya wahadhiri na wafanyikazi wa chuo kikuu cha Moi kusitisha mgomo wao uliodumu miezi mitatu, miungano ya wafanyikazi hao imetangaza kurejelea mgomo wao mara moja kuanzia leo. Katibu wa muungano wa uasu tawi la moi Dkt Busolo Wekesa ametoa tangazo hilo leo jijini Eldoret kwa kile anachosema ni mapuuza ya kutekeleza mkataba wa makubaliano uliotiwa saini mwaka jana. licha ya kukiri kwamba wanajutia hatua hiyo, wafanyikazi hao wanasema hawana njia nyingine ya kupiganiaa haki zao isipikuwa kuitisha mgomo.