Wahaiti waukimbia mji kutokana na mapigano kati ya polisi na magenge ya wahalifu

  • | VOA Swahili
    136 views
    Wananchi wa Haiti katika mji mkuu wa Port-au-Prince wako mbiyoni kwa wiki nzima hivi sasa bila ya kujuwa wapi kwenda kutokana na mapigano kati ya magenge ya uhalifu na polisi. Ghasia hiso zilizuka wiki moja iliyopita na kuilazimisha serikali kutangaza hali ya dharura, na Marekani kuwaondowa raia wake kuanzia siku ya Jumapili. Hali katika nchi hiyo ya Caribean inaripotiwa kuwa mbaya sana na kuisababisha Jumuia ya kimataifa kueleza wasi wasi wake na kutoa wito wa kusitisha ghasia na kudumisha amani. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.