Wahalifu walionaswa wakipora mali wasakwa

  • | KBC Video
    143 views

    Idara ya upelelezi wa jinai inawasaka wahalifu waliodai kuwa waandamanaji lakini wakanaswa kwenye picha za CCTV wakipora na kuvunja biashara kadha katikati ya jiji la Nairobi. Kwenye ujumbe katika kitandazi cha X, idara hiyo inayoongozwa na Mohammed Amin ilisisitiza kwamba hata ingawa wakenya wana haki ya kuandamana, baadhi ya waandamanaji walichukua fursa ya hali tete na kuvunja maduka kwenye barabara ya Ronald Ngala ambapo walipora mali. Na jinsi Abdiaziz Hashim anavyotuarifu, maafisa wa upelelezi wamewahimiza Wakenya kutoa taarifa kuhusu watu ambao picha zao zilinaswa kwenye kamera za CCTV wakitekeleza uhalifu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive