Wahudumu wa afya watumia vyakula vya kiasili kakamega

  • | Citizen TV
    445 views

    Wahudumu wa afya kutoka kaunti ya Kakamega sasa wameanza hamasiho kwa wakazi wa eneo hilo, kutumia vyakula vya kiasili ili kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto. Kulingana na takiwimu kutoka idara ya afya, asilimia 18 ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 walionyesha dalili za utapiamlo na kuathiri malezi yao. Hata hivyo kubuniwa kwa menyu maalum ya shilingi kumi na saba kumechangia katika kupunguza visa hivyo. Laura Otieno na taarifa kamili.