Waislamu sehemu mbalimbali waanza mfungo wa Ramadhan

  • | Citizen TV
    830 views

    Waislamu katika sehemu mbalimbali duniani wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan hii leo. Katika baadhi ya maeneo maandalizi ya mwezi huo mtukufu yanaendeelea, baadhi ya waumini wakijiandaa kuanza mfungo siku ya Jumapili. Na kama anavyoarifu Abdushakur Aboud wa Sauti ya America, waumini wa dini ya kiislamu hujizuia kula na kunywa mchana kwa mwezi moja na kutumia wakati wao mwingi kwenye ibada na kuwajali wasiojiweza.