Wakaazi wa Basuba, Lamu wapata msaada

  • | Citizen TV
    378 views

    Nyuso zenye furaha na bashasha zilishuhudiwa miongoni mwa wakaazi wa Basuba ,kijiji kilichoko maeneo ya ndani ya msitu wa Boni, Lamu baada ya wahisani kujitokeza na kuwaletea chakula cha futari. Chakula hiki kimewafikia wiki moja baada ya Runinga ya Citizen kuangazia masaibu yao. Watu hao walilazimika kula matunda ya mwituni kama chakula cha futari katika mwezi huu wa Ramadhan.