Wakaazi wa Irunduni, anakotoka Kindiki wataka mchakato wa kumuondoa Gachagua ukamilishwe

  • | Citizen TV
    3,236 views

    Wakazi wa kijiji cha Irunduni wameelezea kusononeshwa kwao na uamuzi wa korti kusitisha mchakato wa aliyeteuliwa kuwa naibu rais Kithure Kindiki kushika hatamu afisini humo. Wakazi hao wanasema kuwa walikuwa wamejiandaa kwa sherehe kemkem ila matumaini yao yalififia kufuatia ammri ya mahakama. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, wakazi hao bado wameelezea imani yao kuwa Kindiki hatimaye atachukua hatamu na kuwa naibu rais.