Wakaazi wa Mtwapa 001 walalamikia mabwenyenye wananyemelea ardhi yao

  • | Citizen TV
    320 views

    Wakazi wa kipande cha ardhi cha mtwapa 001 eneo la mtepeni walifanya maandamano kulalamimka kuhangaishwa na mabwenyenye na maafisa wa polisi kwenye ardhi wanayodai ni ya mababu zao. Wakazi hao waliwasha moto na kudai kuwa mbunge wa kilifi kusini ken chonga na msaidizi wake victor katana wamekuwa wakiwafurusha kutoka shamba hilo. Hata hivyo wawili hao wamekana madai hayo huku kamishna wa polisi victor kamondei akisema wapo walaghai wanaovamia mashamba na kutatiza amani kaunti ya kilifi