Wakaazi wa Shanga Ishakani wanalalamikia kukosa maji

  • | Citizen TV
    135 views

    Wakaazi wa Shanga Ishakani katika eneo bunge la Lamu Mashariki, Wadi ya Faza, wanalamikia ukosefu wa maji ambao umetatiza shughuli zao za kila siku, ikiwemo masomo. Kulingana na wakaazi hao, wamekuwa wakitumia maji ya mvua yaliyohifadhiwa katika majabia, lakini kwa sasa maji hayo yamekwisha na wanalazimika kuenda umbali wa kilomita 10 katika kijiji jirani cha Siyu kutafuta maji. wanalalamika kuwa mtungi w alita ishirini huwagharimu shilingi hamsini. Aidha, wakaazi hao wameiomba serikali ya kaunti ya lamu kuingilia kati na kuwasambazia maji kwa kutumia magari ya kubebea maji ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku bila matatizo.