Wakaazi wa Tabriz wakiomboleza kifo cha marehemu Raisi

  • | VOA Swahili
    265 views
    Kikundi kikubwa cha watu kilikusanyika katika mji wa Iran wa Tabriz Jumatatu (Mei 20) baada ya helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Iran Ebrahim Raisi na watu wengine saba kuanguka (Mei 19) ilipokuwa inavuka eneo la mlima lililokuwa na ukungu mkubwa. Baadhi ya watu walionekana wakilia, wakati wengine wakibeba mabango yaliyokuwa na picha za Raisin a Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian. Waliokufa katika ajali hiyo ni pamoja na gavana wa Mkoa wa Azerbaijan Mashariki na kiongozi mwandamizi wa kidini kutoka mji wa Tabriz. Shirika la habari la Reuters lilifanikiwa kuthibitisha eneo hilo kutokana na majengo, kuta, na barabara na alama zake (ambazo zilionekana katika kanda ya video nyimgine iliyokuwa inaonyesha maeneo yaliyofanana) ambayo ililingana na picha za satellite za eneo hilo. Khamenei alitangaza siku tano za maombolezo ya umma na kuthibitisha kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Mohammad Mokhber kuwa ni kiongozi wa mpito wa kitengo hicho cha watendaji wa nchi hiyo. Iran hivi sasa ina kipindi cha siku 50 kamili kabla ya uchaguzi wa rais lazima kufanyika kumchagua mrithi wa Raisi. - Reuters #iran #tehran #ebrahimraisi #waziri #mamboyanje #ajali #helikopta #voa #voaswahili #tabriz