Wakazi wa Angurai huko Teso Kaskazini wakosa maji

  • | Citizen TV
    73 views

    Wakazi wa wadi ya Angurai Mashariki katika eneo bunge la Teso Kaskazini kaunti ya Busia wameitaka serikali ya kaunti ya Busia kuharakisha uzinduzi wa mradi wa maji wa kolanya ili kuwawezesha kupata bidhaa hiyo muhimu. Mradi huo wa maji ulioko katika shule ya upili ya kitaifa ya wasichana ya kolanya na uliogharimu shilingi milioni 25, unanuiwa kunufaisha familia zaidi ya 2,500 mbali na taasisi tano za elimu katika sehemu hiyo...gavana wa busia paul otuoma ameeleza kuwa wamegeukia matumizi ya mitambo ya sola inayotumia miale ya jua kusambaza maji ili kupunguza gharama ya nguvu za umeme, akiwataka wakazi kuwa na subira.