Wakazi wa Entanda, Kitutu Chache Kaskazini, wateketeza nyumba za mshukiwa wa mauaji

  • | Citizen TV
    691 views

    Wanakijiji eneo la Entanda Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii wameteketeza nyumba tatu za mshukiwa wa mauaji ya mzee mmoja eneo hilo . Familia ya marehemu, David Osero inalalama kwamba mmoja wa washukiwa aliyeachiliwa huru anapaswa kusalia korokoroni hadi kesi hiyo ikamilike. Kamanda wa polisi wa Marani Emanuel Rono ametoa taarifa kuhusu hali hiyo, akisema idara ya usalama pamoja na mahakama itahakikisha haki imetendeka.