Wakazi waandamana kulalamikia ubovu wa barabara

  • | Citizen TV
    243 views

    Wakazi wa kijiji cha Limtidi kaunti ya Kisumu walifanya maandamano hii leo kulalamikia ubovu wa barabara ya Muhoroni kuelekea Kericho. Wakazi hao waliwashutumu vikali viongozi wa eneo hilo kwa kuwatelekeza, huku hali mbovu ya barabara ikisitisha shughuli za kibiashara baina ya kaunti za Kisumu na Kericho. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, hali ya usalama pia imekuwa tete huku wahalifu wakijificha katika mashimo yaliyoko barabarani.