Wakenya wamezoa medali nyingi kwenye shindano la Miereka

  • | Citizen TV
    580 views

    Wapigaji miereka wa Kenya wamenyakuwa idadi kubwa ya medali kwenye siku ya mwisho ya michuano ya Afrika Mashariki yaliyomalizika nairobi hapo jana.. Katika siku ya pili ambayo ilikuwa maalum kwa miereka ya ufukweni, kenya ilishinda medali zote katika vitengo vya kilo 70 na kilo 80 kwa wanaume. Omary musa wa tanzania alimshinda mkenya alphonse gumba na kunyakuwa dhahabu katika pigano la kilo 90 kwa wanaume huku gloria niyonkuru wa burundi akishinda dhahabu katika kilo 60 wanawake dhidi ya emma nekesa wa kenya. Jane kwamboka wa kenya nae alinyakua dhahabu ya kilo 70 dhidi ya vihanshy simran wa mauritius. Michuano hiyo ya siku mbili iliwavutia zaidi ya wapiganaji 50 kutoka mataifa sita.