Wakenya waraiwa kutunza wakongwe

  • | Citizen TV
    739 views

    Ombi la kila binadamu kwa mola ni kuishi miaka mingi duniani lakini kwa wakongwe wengi nchini maisha yao ya uzeeni si ya kuridhisha ,jamii zao zikichukuilia uwepo wao kama mzigo ,hatimaye kutelekezwa bila msaada wowote. Hali hii imewachochea wakazi wa Kiptuiya eneo bunge la Chesumei kujitokeza kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwalinda wakongwe kwa kuhakikisha wamepata lishe bora, mavazi na kuwapa upendo.