Wakimbizi wa DRC wanaovuka mto hatari kwenda Burundi

  • | BBC Swahili
    1,174 views
    Zaidi ya watu elfu hamsini wameyakimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Burundi, wakihatarisha maisha yao kwa kuvuka mto Rusizi kwa kuogelea. Zaidi ya watu ishirini wamefariki dunia wakijaribu kuuvuka mto huo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Wale ambao wamefanikiwa kuvuka wanasema kama wangeendelea kusalia DRC, wangelazimishwa kujiunga na kundi la waasi la M23 - madai ambayo BBC haijathibitisha. Lakini huku M23 ikiendelea kuteka maeneo zaidi mashariki mwa Congo, kuna hofu kuwa wakimbizi hawako salama hata katika nchi jirani ya Burundi.