Wakulima kusambaziwa magunia milioni mbili za mbolea

  • | Citizen TV
    174 views

    Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati unaofaa msimu wa upanzi ukikaribia. Akizungumza huko Chepseon eneo bunge la Kipkelion Mashariki wakati wa ufunguzi wa sehemu ya uzambasaji wa mbolea, katibu katika wizara ya kilimo Dkt.Paul Ronoh ametangaza kuwa mpango huo utaendelea kwa muda wa miezi miwili ili kuwasaidia wakulima kuzalisha vyakula na kuleta utoshelevu wa lishe nchini. Aidha serikali imetoa ruzuku kwa kampuni ya kuzalisha mbegu za mahindi ili kuwezesha uzalishaji wa mbegu za kutosha na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbegu kwa bei nafuu.