Wakulima nchini wahangaika wakitafuta mbolea ya upanzi

  • | Citizen TV
    587 views

    Huku msimu wa upanzi ukiendelea kufikia kikomo, wakulima katika maeneo mengi nchini bado wanahangaika kupata mbolea ya upanzi, baadhi sasa wakilazimika kununua mbolea ya bei ghali kabla ya kupitwa na wakati. Mahangaiko ya wakulima yanajiri huku wizara ya kilimo ikikiri kwamba kumekuwepo na changamoto ya kusafirisha mbolea, ikiahidi kwamba kufikia jumatatu maghala ya NCPB kote nchini yatakuwa na mbolea ya kutosha kufanikisha muhula wa upanzi.