Wakulima wa chai walalamikia bonasi kidogo Gusii

  • | Citizen TV
    309 views

    Wakulima kutoka eneo la Gusii wamelalamikia malipo duni ya bonasi ya majani chai. Wakizungumza kwenye hafla za kukusanya maoni zilizoandaliwa na kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa kule Nyansiongo na Kiamokama katika kaunti za Nyamira na Kisii, wakulima hao wamedai kubaguliwa kimalipo na bodi ya majani chai nchini.