Wamalwa: Tutazidi kukosoa serikali

  • | Citizen TV
    1,232 views

    Kinara wa DAP Kenya, Eugene Wamalwa, amekashifu matamshi ya Rais William Ruto ya hapo jana ambapo rais alisema viongozi wa upinzani ni matepeli, akisema matamshi hayo hayafai kutolewa na mtu mwenye hadhi ya Rais. Wamalwa amesema kuwa upinzani utaendelea kumkosoa rais na serikali ili iwajibike ipasavyo.Akizungumza katika eneo la Kapsitwet huko Kitale, kwenye mazishi ya Matthew Wandati, mwanafunzi wa Chuo cha Strathmore aliyepatikana ameuawa, wamalwa amesema kuwa upinzani utaendelea kuwakumbusha wananchi kuhusu athari za sera zinazotekelezwa na serikali na kuhakikisha kuwa maslahi ya Wakenya yanafanywa kipaumbele.