Wamiliki wa biashara jijini Nairobi waelezea kusikitishwa na maandamano yanayoendelea

  • | K24 Video
    19 views

    Wamiliki wa biashara jijini Nairobi wameelezea kusikitishwa kwao na maandamano yanayoendelea, ambayo yamedumu kwa takriban miezi miwili. Maandamano hayo ambayo awali yalikuwa ya amani, yamezidi kuleta usumbufu na kusababisha hasara kubwa ya kifedha kwa wafanyabiashara, ambao wanapambana na kupungua kwa wateja na pia wanakabiliwa na tishio la uporaji, hali inayowalazimu wengi kufunga maduka yao.