Wanafunzi aliyeugua saratani apata A- KCSE

  • | Citizen TV
    437 views

    Huku wanafunzi waliopata alama za kuridhisha kwenye mtihani wa KCSE mwaka 2024 wakiendelea kusherehekea, mtahiniwa mmoja aliyekosa masomo kwa mwaka mmoja baada ya kuuugua saratani amesherehekewa kw akupata alama ya A-. Danson Baragu aliyekuw aakisomea katika shule ya wavulana ya Baricho kaunti ya Nyeri, alikosa masomo ya kidato cha pili na cha tatu alipokuwa akipokea matibabu ya saratani. Kamau Mwangi alizuru hospitali ya rufaa ya Nyeri ambako Danson alindaliwa sherehe na wauguzi.