Wanafunzi sita waaga dunia Kitui baada ya kugongwa na gari

  • | KBC Video
    24 views

    Maafisa wa Polisi kaunti ya Kitui wanachunguza vifo vya wanafunzi sita waliofariki papo hapo kufuatia ajali ya barabarani katika kituo cha biashara cha Wiitu kwenye barabara ya Kitui kuelekea Kibwezi. Watu hao sita waligongwa na gari aina ya Probox walipokuwa wakitembea kando ya barabara wakielekea katika shule ya msingi na sekondari ya Kyoani. Huku hayo yakijiri, watu wawili walifariki jana jioni katika kituo cha biashara cha Kaburengu kaunti ya Kakamega kufuatia ajali kwenye barabara ya Eldoret kwenda Malaba.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive