Wanafunzi wa kike 208 Lungalunga wapata mafunzo

  • | Citizen TV
    232 views

    Wanafunzi wa kike 208 kutoka shule za msingi na sekondari msingi eneo la Lungalunga katika kaunti ya Kwale wamenufaika na mradi wa masomo wa kuimarisha kusoma na kuandika.Wanafunzi hao kutoka shule 5 za Vanga wamekua kwenye mpango unaohamasisha jamii, walimu na wanafunzi kuhusu jinsi ya kuimarisha elimu ya mtoto wa kike. Mradi huo pia umeshinikiza uwajibikaji wa jamii kwenye maswala ya usafi wa hedhi safi na mbinu za kukabili dhulma za kijinsia. Lawrence Ng'ang'a anaarifu zaidi kutoka Kwale