Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Lugulu wanyimwa matokeo kwa madai ya udanganyifu

  • | K24 Video
    79 views

    Wanafunzi 699 kutoka shule ya upili ya kitaifa ya wasichana ya Lugulu wamejawa na wasiwasi na taharuki baada ya matokeo yao ya mtihani wa kitaifa wa KCSE wa mwaka 2024 kuzuiliwa kwa madai ya udanganyifu. Huku uchunguzi ukiendelea, tulizungumza na mmoja wa wanafunzi walioathirika. Nancy ambaye si jina lake halisi na anahofia kuwa ndoto yake ya kutaka kuwa daktari wa matibabu haitatimia. .