Wanafunzi walionufaika na mpango wa Equity Wings to Fly wakutana

  • | Citizen TV
    132 views

    Afisa Mkuu wa Benki ya Equity Dkt James Mwangi, leo ameongoza hafla ya kuwahamasisha wanafunzi waliofaidi mpango wa elimu wa benki hiyo wa Wings to Fly. Kongamano hilo lililowaleta pamoja wanafunzi 1800 wa Kidato cha Tatu na Nne kutoka sehemu mbalimbali nchini lilitoa fursa ya hamasisho zaidi kuhusu elimu. Wanafunzi kutoka maeneo ya Mashariki walikutana Machakos huku vikao sawia vikiandaliwa eneo la Pwani, Rift Valley, Magharibi na Nyanza. Vikao hivi pia viliwahamasisha wanafunzi kuhusu changamoto za ulimwengu wa kisasa, hasa kupitia teknolojia na uongozi.