Wanafunzi watatu waangamia kwenye ajali ya barabarani Nyakach

  • | KBC Video
    567 views

    Wanafunzi watatu wa shule ya wavulana ya malazi ya Ober iliyoko katika kaunti ya Homabay walifariki papo hapo huku wengine tisa wakijeruhiwa kufuatia ajali kwenye barabara ya kutoka Sondu kuelekea Katito katika eneo la Nyakach, kaunti ya Kisumu. Mbali na hayo, wanafunzi wawili kutoka shule ya upili ya Mbita humo humo katika kaunti ya Homabay wanaendelea kuuguza majeraha katika hospitali ya matibabu maalum ya Homabay baada ya kugongwa na gari la kibinafsi kwenye barabara ya kutoka Mbita kuelekea Sindo. Wycliffe Oketch ana taarifa hii kwa kina.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive