Wanahabari wahimizwa kutoa taarifa sahihi za mazingira

  • | KBC Video
    6 views

    Wadau katika sekta ya vyombo vya habari wameelezea wasiwasi wao kuhusiana uzambazaji wa taarifa potovu kuhusu mabadiliko ya hali ya anga,wakisema hii inachangiwa na ukosefu wa mafunzo maalum kuhusu sayansi ya hali ya anga miongoni mwa wanahabari. Wadau wanahusisha hali hii hi ya kutamausha na uwasilishaji wa taarifa zisizo za ukweli au ufafanuzi kupita kiasi maswala mazito yanayofungamana na mazingira. Akizungumza jijini Nairobi wakati wa maadhimisho ya siku ya Redio ulimwenguni, katibu katika idara ya utangazaji na mawasiliano Proffesa Edward Kisiang'ani alisisitiza haja ya utekelezaji mipango maalum ya mafunzo ili kuwapa wanahabari maarifa ya jinsi ya kuandika taarifa sahihi kuhusu tabianchi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive