Wanajeshi

  • | VOA Swahili
    1,815 views
    Gavana wa Kaunti ya Kisumu, Kenya, amejitokeza kulaani utekaji uliofanyika. Amesema wazi kuwa serikali ya kaunti haikuhusishwa. Hayo yameelezwa na Meya wa Mji wa Kampala,Elias Lukwago ambaye anasema gavana huyo pia anataka maelezo kamili kujua kwa nini wanajeshi wa Uganda waliivamia Kisumu na kuwakamata "wenzetu 33." Naye makamu wa rais wa chama cha upinzani Uganda FDC, Salam Musumba alisema: Viongozi hao wametekwa, katika karne hii ya 21 wametekwa, Tutawasilisha barua yetu ya malalamiko Ubalozi wa Kenya nchini Uganda, alieleza. "Na kuwajulisha kuhusu utekaji kinyume cha sheria na wa kikatili Utekaji wa viongozi 36 wa chama cha FDC," makamu rais alieleza. Kwa mujibu wa uongozi wa FDC wakati wakikamatwa viongozi hao walikuwa katika Kituo cha Umma cha Uchungaji mjini Kisumu ambako walikuwa wanahudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo wa mikakati ya masuala ya siasa kwa wiki moja. #uganda #kenya #kisumu #fdc #upinzani #meya #kampala #polisi #ugaidi #ibrahimssemujjunganda