Wanajeshi waliokimbia vita DRC washtakiwa

  • | BBC Swahili
    6,986 views
    Makumi ya wanajeshi wa DRC wamefunguliwa mashtaka mjini Bukavu, mkoani Kivu Kaskazini. Wanajeshi hao wanashtakiwa kwa kutoweka wakati wa makabiliano na waasi wa M23. Waendesha mashtaka wa jeshi wanasema wanajeshi hao pia wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji, ubakaji na wizi baada ya watu 9 kuuawa mjini Bukavu siku ya Ijumaa. Huku hayo yakijiri, hali ya kawaida imeanza kurejea katika mji wa Goma huku shule na vyuo vya masomo vikifunguliwa tena.