Wananchi wawakabili wanaodaiwa kuwa watekaji nyara

  • | Citizen TV
    9,252 views

    Ongezeko la utekaji nyara bila majibu kutoka kwa asasi za usalama limewafanya raia kuwa macho punde wanaposhuhudia watu wanaodhaniwa kuwa watekaji nyara wakijaribu kuwateka wananchi. Matukio wakati wa utekaji nyara wa mhariri kutoka tanzania, pamoja na kufumaniwa kwa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare za kazi na ambao walidinda kujitambulisha kwa raia katika kaunti za Nakuru na Kirinyaga kumeibua taharuki.