Wanyama wawekwa alama mbuga ya Tsavo

  • | KBC Video
    12 views

    Shirika la kuhifadhi wanyama pori-KWS limeanza shughuli ya kuwaweka alama na vifaa vya kielektroniki vifaru katika mbuga ya kitaifa ya Tsavo ili kulinda idadi ya wanyama hao. Teknolojia hiyo inanuiwa kutambua na kuwalinda vifaru katika mbuga hiyo dhidi ya uwindaji haramu na kupotea kwa makazi yao.Akigusia shughuli hiyo, waziri wa utalii na wanyama pori Rebeca Miano amekariri umuhimu wake akisema takwimu zitakazokusanywa zitasaidia kutekeleza mkakati wa mwaka-2022/2026 wa kuhifadhi vifaru weusi. Aidha, waziri Miano amesema teknolojia hiyo itarahisisha kufuatilia mienendo ya vifaru na kuhakikisha wanalindwa ipasavyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive