Watu kumi, wakiwemo wanawake watatu na watoto watatu, wamezikwa leo Alhamisi baada ya kuuwawa katika mashambulizi ya Israel katika miji ya kusini ya Khan Younis and Rafah.
Mohammad Abu Huweij amesema mke wake na watoto watatu walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa huko Khan Younis jana jioni.
Sheikh wa Kiislamu aliongoza sala ya mazishi pamoja na kundi la wanaume waliokuwa nje ya Hospitali ya Nasser huko Khan Younis, wakati wanawake na wasichana walikuwa wakilia kabla ya miili hiyo kuchukuliwa kwenda kuzikwa.
Wizara ya Afya ya Gaza inasema zaidi ya Wapalestina 41,000 wamaeuawa katika eneo hilo Tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7. Wizara hiyo haikutenganisha ni wapiganaji wangapi na raia wangapi katika hesabu waliyotoa.
Israel inasema imewaua wanamgambo 17,000 bila ya kutoa ushahidi.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu amelishutumu jeshi la Israel kwa kupiga shule, wafanyakazi wa kibinadamu na raia huko Gaza ikiwa ni dalili ya kuongezeka kwa wasi wasi wa Marekani kwa mashirika wake wa karibu wakati vita vinaelekea mwaka mmoja.
Jeshi la Israeli lilianzisha moja ya mashambulizi makubwa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israeli kwa miezi kadhaa sasa Jumatano (August 28), na kuuwa watu 19, wakiwemo makamanda wa Hamas na Islamic Jihad.
Israel imekuwa ikitekeleza kile imekitaja kama operesheni ya kijeshi karibu kila siku katika Ukingo wa Magharibi, tangu Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas walipofanya shambulizi kutokea Gaza na kusababisha vita vikali vinavyoendelea.
Israel imesema kwamba operesheni yake ya kijeshi ina lengo la kuwamaliza nguvu wanamgambo wa Hamas na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wake
- Vyanzo mbalimbali
#wapalestina #jeshi #israel #hamas #shambulizi #maziko #rafah #khanyounis #palestina #voa #voaswahili
21 Apr 2025
- As an at-times unwitting star on social media, Pope Francis knew how to exploit the internet to preach the gospel, broadening the Church's appeal while modernising its communications.
21 Apr 2025
- US Defense Secretary Pete Hegseth fought back Monday -- with White House support -- against another scandal over his reported use of Signal to discuss airstrikes on Yemen, this time with his wife, brother and lawyer.
21 Apr 2025
- President William Ruto will visit Beijing and meet with President Xi Jinping as reciprocal trade tariffs between America and Beijing deepen, and shockwaves in the aftermath of the tariffs rip through the global markets.
21 Apr 2025
- With Pope Francis’s death, the immediate running of the Vatican is now in the hands of one cardinal, Dublin-born Cardinal Kevin Farrell. Known as the Camerlengo, and appointed by the pope, it is he who will lead meetings to determine the date of Francis…
21 Apr 2025
- Some cardinals who are being talked about as "papabili" to succeed Pope Francis, whose death at the age of 88 was announced by the Vatican on Monday.