Wapiga kura wamekaa katika foleni kwa saa mbili DRC

  • | VOA Swahili
    310 views
    Upigaji kura ulianza huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano huku vituo vya kupiga kura vikichelewa kufunguliwa katika mji mkuu, Kinshasa. Mwandishi wa VOA Abdushakur Aboud alikuwa katika kituo cha kupiga kura ambapo wapiga kura walikuwa wamesubiri kwa zaidi ya saa mbili ili kituo kifunguliwe. Takriban raia wa Congo milioni 44 wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi wa rais, bunge na mikoa. Kero mbalimbali zimeripotiwa katika sehemu nyingine za nchi, ikiwemo mashariki mwa DRC, ambako watu walisema hawakuona majina yao katika orodha ya wapiga kura. (VOA/Reuters/AP) #drc #rwanda #congo #felixtshisekedi #tshisekedi #drcelection #drcelection2023 #kinshasa #voa