Wapiga kura wavutana na vikosi vya usalama nje ya kituo cha kupiga kura Kinshasa

  • | VOA Swahili
    490 views
    Upigaji kura ulianza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano huku vituo vya kupiga kura vikichelewa kufunguliwa katika mji mkuu, Kinshasa. Mwandishi wa VOA Abdushakur Aboud alikuwa katika kituo kimojawapo Kinshasa ambapo wapiga kura wenye hasira waliwasukuma na kuwafokea walinzi wa usalama kutokana na kukata tamaa. Takriban Wakongo milioni 44 wamejiandikisha kushiriki katika upigaji kura wa rais, wabunge na mikoa. Baadhi ya kero zimeripotiwa katika maeneo mengine nchini humo, ikiwemo mashariki ya DRC, ambapo watu walieleza hawakuweza kuyaona majina yao katika orodha ya wapiga kura. Waangalizi wa kujitegemea wa uchaguzi na wakosoaji walitahadharisha siku kadhaa kabla ya uchaguzi kuwa dosari mbalimbali zitaweza kuhatarisha uhalali wa matokeo ya uchaguzi. ⁣ (VOA Africa/Reuters/AP)⁣ #drc #rwanda #congo #felixtshisekedi #tshisekedi #drcelection #drcelection2023 #kinshasa #voa