Wapinzani wakuu watatu wa Tshisekedi wamepiga kura asubuhi

  • | VOA Swahili
    2,134 views
    Kati ya Shauku, hasira na vurugu, wananchi wa DRC wanafanya kila wawezalo kupiga kura Jumatano katika uchaguzi uliokuwa na mashaka ambapo rais anayemaliza muhula wake, Felix Tshisekedi, anachuwana na upinzani uliogawanyika ambao haraka umedai kuwepo “mapungufu”. “Ni vurugu tupu,” Martin Fayulu alisema pia baada ya kupiga kura Kinshasa, kwa mara nyingine tena akiituhumu Tume ya Uchaguzi (Ceni) kutaka kwa hali yoyote “kumpitisha” Felix Tshisekedi. Moise Katumbi, ambaye alipiga kura katika ngome yake ya Lubumbashi, aliwataka wapiga kura “kufuatilia” zoezi la kuhesabu kura “mpaka mwisho.” Katika jimbo la jirani la Ituri, ambalo pia lilikumbwa na ghasia kutoka vikundi vyenye silaha, waandamanaji, wakiwemo watu waliokoseshwa makazi kwa sababu ya vita kulingana na vyanzo mbalimbali vya eneo, waliharibu kituo cha kupigia kura, “Walivunja kila kitu,” amelalamika afisa moja wa Ceni katika eneo hilo. Source: AFP #drc #rwanda #congo #felixtshisekedi #tshisekedi #drcelection #drcelection2023 #kinshasa #voa #martinfayulu #moisekatumbi #denismukwege