Waridi wa BBC: Mwanamke pekee anayeendesha feri nchini Kenya

  • | BBC Swahili
    1,428 views
    Mishi Iddi Omar nahodha wa kipekee mwanamke anayeendesha feri kubwa zinazosafirisha magari, abiria na bidhaa tofauti katika kivuko cha Likoni na kisiwa cha Mombasa eneo la Pwani nchini Kenya. Huendesha moja ya feri nne kuu na safari thelathini na nne kila anapokuwa zamu. ''Kwa kweli inahitaji ukakamavu mwingi kujiamini , kuwekeza katika masomo na kutoa muda wangu mwingi kufanya kazi hii" alisema. Anasema miongoni mwa changamoto alizowahi kukutana nazo ni chombo kupoteza mitambo yake ya pande zote mbili ghafla akiwa katikati mwa bahari kwenye kina kirefu. Mwanahabari wetu Anne Ngugi alizungumza na Mishi Idd #bbcswahili #waridiwabbc #Kenya