Washikadau katika sekta ya uchimbaji madini wataka kujumuishwa kwenye utunzi wa sera

  • | Citizen TV
    181 views

    Washikadau mbalimbali katika sekta ya Uchimbaji wa madini kutoka ukanda wa Nyanza wanatoa wito kwa serikali kuwajumuisha wachimbaji wadogo katika maswala ya sheria zinazoendesha sekta hiyo kando na njia mwafaka wa kukabili changamoto wanazokumbana nazo Wakizungumza mjini Kisumu katika hafla ya uzinduzi wa utafiti huo, wadau walitoa wito kwa serikali kuipa kipaumbele mbinu bora za kutoa leseni kwa wachimbaji madini.Aidha serikali imehimizwa kuziba mianya inayotumiwa na baadhi ya wachimbaji madini haramu ambao wanachangia kupotea kwa mamilioni ya pesa ambazo zingekusanywa kama ushuru.