Washikadau wa elimu watoa hamasa kwa wanafunzi kudumisha nidhamu shuleni

  • | Citizen TV
    348 views

    Washikadau mbalimbali katika sekta ya elimu wamekongamana eneo la Mugirango Kusini kwa lengo la kutoa hamasisho kwa wanafunzi wa shule za upili kama njia mojawapo ya kukabili visa vya kuteketeza mabweni ya shule hususan muhula wa tatu. Wakizungumza katika Shule ya upili ya Wavulana ya Nduru, Naibu Chansela wa chuo Kikuu cha Egerton, Profesa Isaac Kibwage, walimu wakuu wameshauriwa kufanya mikutano ya mara kwa mara na wanafunzi wao na kuwapa fursa ya kujielezea iwapo kuna changamoto miongoni mwao.Aidha washikadau katika sekta hiyo wameapa kuhusisha washauri nasaha mara kwa mara kupata suluhu ya mapema kwa maswala yanayozidi kuzonga wanafunzi wakiwa shuleni ili kuzuia rabsha katika taasisi hizo za elimu.