Washukiwa watatu washtakiwa kwa wizi wa kimabavu mjini Narok

  • | Citizen TV
    1,215 views

    Washukiwa watatu wa wizi wameshtakiwa katika mahakama ya Narok kwa makosa ya wizi wa kimabavu, uharibifu wa mali na kupatikana na vifaa vya elektroniki vilivyoibwa. Wezi hao ambao waliokamatwa ijumaa iliyopita katika maeneo ya Total na Macedonia, walifikishwa mbele ya Hakimu Hezron Nyaberi na kukanusha mashtaka yote. Aidha walipatikana na mitungi ya gesi, simu za rununu na kipatakilishi, vyote hivyo vikisemekana kuwa mali ya wizi.Washukiwa watazuiliwa hadi tarehe 21 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakaposikizwa tena. Polisi bado wanawasaka washukiwa wengine watatu waliotoweka baada ya wenzao kufumaniwa.