Wasiwasi watanda kuhusu Marekani kujiondoa

  • | Citizen TV
    12,267 views

    Uamuzi wa Rais mpya wa Marekani, Donald Trump, kuwa Marekani itajiondoa kwenye shirika la afya duniani -WHO, kumezua taharuki , haswa kuhusiana na ufadhili wa mipango ya afya katika mataifa mengi duniani. Shirika hilo limemwomba rais Trump kubadili mtazamo wake kuhusiana na uamuzi huo. haya ni huku Wataalamu wa afya ya umma nchini wakionya kuwa kujiondoa kwa Marekani kutakuwa na madhara makubwa katika vita dhidi ya majanga ya kitaifa ya kiafya.