'Wateja wengi wa kipato cha chini wanapenda dagaa'

  • | BBC Swahili
    207 views
    Zuio la kuvua dagaa kwa siku nane kila baada ya wiki tatu katika Ziwa Victoria Nchini Tanzania limesababisha uhaba mkubwa wa dagaa katika maeneo mbalimbali. Zoezi hili hufanyika na mamlaka ya ziwa hilo, ili kuruhusu dagaa kuzaliana kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uvuvi haramu. Lakini baadhi wanahoji kwanini zoezi hilo linahusisha dagaa peke yake na kuacha aina nyingine ya Samaki ziwani humo? Mwandishi wa BBC @mcdavid_nkya_ ametembelea Ziwa Victoria Mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na kuandaa taarifa ifuatayo. 🎥 @eagansalla_gifted_sounds #bbcswahili #tanzania #mwanza Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw