Watoto wengi Samburu huzaliwa na maradhi ya mtoto wa jicho

  • | Citizen TV
    291 views

    Visa vya watoto kuzaliwa na maradhi ya mtoto wa jicho kaunti ya Samburu vimetajwa kuchangiwa na wanawake wajawazito kukosa kufika kliniki. Tatizo hilo husababisha kupofuka iwapo hautatambuliwa mapema na kutibiwa. Hali hiyo imesababisha watoto wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na mitatu kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Samburu. Bonface Barasa na taarifa hiyo.