Watu waichomoa miili iliyokwama katika kifusi Rafah

  • | VOA Swahili
    220 views
    Wapalestina walikusanyika katika eneo ambalo Israeli ilifanya mashambulizi ya anga huko Rafah, kusini mwa Gaza, Jumatano (Januari 24), na kusaidiana kuichomoa miili kadhaa iliyokuwa ndani ya kifusi. Eneo hilo, ambalo liko mpakani na Misri, limefurika zaidi ya nusu ya watu milioni 2.3 wa Ukanda wa Gaza, waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya Israeli na Hamas. “Wapi ni sehemu salama? Hakuna sehemu salama, hakuna chakula na hakuna pakujificha,” alisema mmoja wa wale waliokoseshwa makazi katika eneo la tukio, Um Khaled Baker. Mabomu yaliyofyatuliwa na vifaru yalipiga kituo cha mafunzo cha Umoja wa Mataifa kilichokuwa kimewahifadhi maelfu ya watu waliokoseshwa makazi huko Khan Younis Jumatano, na kuua watu wasiopungua tisa na kujeruhi 75, afisa mwandamizi wa misaada wa UN alisema, wakati majeshi ya Israeli yakielekea mbele zaidi kusini mwa mji wa Gaza, huku watu wengi zaidi wakilazimika kukimbilia Rafah. Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200. Maafisa wa afya wa Palestina walisema watu wasiopungua 25,700 wakazi wa Gaza wameuawa katika vita hivyo, ikiwemo 210 waliofariki katika saa 24 zilizopita, huku maelfu wakihofiwa kuwa wamefukiwa ndani ya kifusi. - Reuters ⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣ ⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #khanyounis