'Watu walikuwa wamelala katika nyumba zao -- watoto, mauaji...'

  • | VOA Swahili
    547 views
    Kanda ya video ikionyesha miili ya Wapalestina waliouawa katika shambulizi la anga la Israel. Ndugu na jamaa wamekusanyika katika Hospitali ya AL-Aqsa Martyrs wakijadili kuhusu shambulizi hilo. Mpalestina, Mohammed Rayyan, ambaye ndugu yake aliuawa anaeleza huzuni na simanzi zake: "Watu walikuwa wamelala katika nyumba zao – watoto, mauaji. Je, hizi ni haki za binadamu wavamizi wanazo zizungumzia? Watoto. Je, huu ndio ubinadamu wanaounadii? Watoto wasiokuwa na hatia; ndege wa peponi. Mvulana huyu ni mtoto pekee kwa baba yake. Kwa baba na mama yake. Mama yake huyu hapa, ameuawa shahidi. Na huyu hapa, tunaamini ni shahidi mbele ya Mungu Mtukufu. Hatuna cha kusema lakini kumshukuru Mungu.” Tangu Hamas ilipofanya shambulizi Oktoba 7, mashambulizi ya Israel huko Gaza yameuwa zaidi ya Wapalestina 35,000, kulingana na maafisa wa afya wa Gaza. Hamas inayoongozwa na watu wenye silaha imeua takriban watu 1,200 na kuwateka watu 253 katika uvamizi wa Oktoba 7 waliofanya ndani ya Israel, kulingana na hesabu iliyojumlishwa na Israel. - Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #helikopta #shambulizi #unrwa #un