Watu watatu waaga dunia baada ya matatu walimokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali

  • | Citizen TV
    3,769 views

    Watu watatu wameaga dunia huku wengine sita wakipata majeraha mabaya baada ya matatu walimokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali kwenye barabara ya Narok - Nakuru. Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi eneo la Narok ya kati John Momanyi amesema ajali ilitokea wakati wa asubuhi pale matatu hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Narok kupoteza mwelekeo baada ya hitilafu ya magurudumu ya nyuma.