Watu watatu wajeruhiwa kwenye uchaguzi wa ODM mashinani kaunti ya Homa Bay

  • | Citizen TV
    296 views

    Watu watatu wanauguza majeraha ya panga baada ya vurumai kuzuka wakati wa uchaguzi wa mashinani wa chama cha ODM kaunti ya Homa Bay Kulingana na kamanda wa polisi eneo la Ndhiwa John Loisa, makundi mawili yalitofautiana wakati wa uchaguzi katika shule ya msingi ya Buche na kusababisha majeraha huku mmoja akikatwa mkono. Aidha uchaguzi huo pia ulichelewa kuanza katika kaunti ya Migori. Chama cha ODM kilianza upigaji kura katika maeneo ya wadi hii leo huku uchaguzi wa wawakilishi wa bunge ukitarajiiwa kufanyika Jumatano