Watu wawili wangali wamekwama ndani ya bomba lililoporomoka Bamburi, Mombasa

  • | Citizen TV
    1,564 views

    Watu wawili wanahofiwa kufariki baada ya kuzama ndani ya bomba la maji taka huko Bamburi eneo Bunge la nyali kaunti ya Mombasa. Maafisa wa kaunti wamekuwa na kibarua kigumu kujaribu kufikia eneo la mkasa na kulazimu kuvunja baadhi ya sehemu za nyumba ili kutoa nafasi ya uokoaji wa wawili hao. Walioshuhudia tukio hilo wanasema hakuna aliyefahamu kuwa sehemu ya banda la kutazama sinema na mpira lilijengwa juu ya bomba la maji taka. Kulingana na serikali ya kaunti bomba hilo lina kina cha zaidi ya futi 100. Uchukuzi pia umeathirika hasa maeneo ya Bamburi mwisho baada ya maafisa wa polisi kufunga sehemu ya barabara hiyo.