Watu zaidi ya mia mbili waathirika na ugonjwa usioeleweka Mugirango Kusini, Kisii

  • | Citizen TV
    3,707 views

    Zaidi ya watu mia mbili wanaoishi katika vijiji vitatu eneo la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii wanaugua ugonjwa ambao maafisa wa afya wameshindwa kuutambua kufikia sasa. Wakazi hao wanalalamikia maumivu makali ya kichwa, kuharisha damu, kutetemeka na dalili zinginezo. Maafisa wa wizara ya afya wamepiga kambi katika mpaka wa Kisii na Migori kutathmini hali na kuchukua sampuli za wagonjwa kwa uchunguzi wa kina. CHRISPINE OTIENO amerejea kutoka eneo hilo na sasa anatuchorea taswira kamili ya hali ilivyo.