Wauguzi waandamana Kakamega na Embu

  • | KBC Video
    92 views

    Wauguzi walioajiriwa chini ya mpango wa afya kwa wote-UHC waliandamana wakielezea kughadhabishwa na kile walichodai kuwa kukosa kwa serikali kuwaajiri chini ya kandarasi za kudumu. Wauguzi hao kutoka kaunti za Kakamega, Bungoma, Busia na Vihiga pia wanashinikiza malipo ya baada ya kipindi cha kuhudumu wakielezea wasiwasi kuhusu hatma yao baada ya serikali za magatuzi kukosa kuwaajiri. Maandamano sawia yalishuhudiwa katika kaunti ya Embu yakiwahusisha wauguzi kutoka kaunti nyingine tano za Meru, Tharaka Nithi, Kirinyaga na Murang’a ambao walilalamikia mazingira duni ya kikazi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive